Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Mkirikiti amepongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa usimamizi mzuri wa Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mhe. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo Kijiji cha Mwada Kata ya Mwada kunakojengwa Hospitali hiyo kwenye ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ktk Wilaya ya Babati. Aidha katika mradi huo ameagiza nyumba za Watumishi zijengwe na Halmashauri ihamasishe wawekezaji kuja kuwekeza katika eno hilo."Mradi huu ni mkubwa ,Halmashauri inatakiwa kujenga majengo mazuri kuzunguka eneo lote la hospitali na kuhamasisha Wawekezaji kuwekeza ktk eneo hilo" amesisitiza kiongozi huyo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.