Halmashauri ya Wilaya ya Babati imeanza kutoa mafunzo ya NAPA kwa ajili ya utambuzi wa Barua za wanafunzi wanaomba mkopo wa Elimu ya juu. Afisa TEHAMA Ndg Devota Mbonamasabo amesema mafunzo hayo yameanza leo katika ukanda wa Dareda, Bashneti na Gallapo na yataendelea katika Tarafa zote. Aidha ametanabaisha kuwa wahusika wa mafunzo hayo ni Watendaji wa Kata, vijjiji na wanafunzi tarajiwa wa vyuo vikuu na akatoa wito wahusika kuhudhuria mafunzo hayo kwani ni muhimu wakati huu ambapo Dunia Iko kwenye mageuzi ya Sayansi na Technolojia . Kwa Upande wake Mtendaji wa Kata ya Ayalagaya Ndg Onesma Lohay ameshukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuwezesha mafunzo hayo kwani uhitaji wa utambuzi kwa wanafunzi hao ni Mkubwa na utaondoa kero ya wanafunzi hao kutembea mwendo mrefu kufuata huduma hiyo .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.