Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, Agosti 8, 2025 ametembelea mabanda mbalimbali kwenye Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Themi Njiro, jijini Arusha, ambapo ametembelea pia mabanda ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati akiwa kama Mgeni wa zamu wa siku hiyo.Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Kaganda ametoa wito kwa vijana kujikita zaidi katika sekta ya kilimo na ufugaji akisisitiza kuwa kuna fursa kubwa sana za kiuchumi kwenye sekta hizo iwapo vijana wataamua kuwekeza muda na maarifa yao.“Mimi mwenyewe pia ni mkulima wa na naona matokeo. Vijana msisubiri ajira tu, jengeni ajira zenu kupitia ardhi yenu, Kuna mikopo inayotolewa na Halmashauri twende tukaipate mikopo hiyo ili tuweze kupata kianzio” amesema Mhe. Kaganda.
Aidha, amewataka vijana kuacha tabia ya kuuza ardhi za familia kwa kisingizio cha kutafuta mtaji wa biashara, na badala yake watumie ardhi hizo kama mtaji wa kuanzisha kilimo biashara chenye tija na endelevu.Vilevile, ametoa rai kwa maafisa biashara kutoka Halmashauri kuwasaidia wafanyabiashara kuongeza thamani ya bidhaa wanazozalisha ili ziweze kupata masoko mapana ya ndani na nje ya nchi.Mhe. Kaganda amewapongeza washiriki wote wa maonesho hayo na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ubunifu na teknolojia katika kilimo ili kuongeza tija na mapato kwa wananchi huku akiwaalika wote ambao Bado hawajafika waje wajifunze
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.