• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Babati District Council
Babati District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango Ufuatiliaji na Takwimu
      • Ardhi mali Asili na Wanyamapori
      • Maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mazingira na Usafi wa Mazingira
      • Afya
    • Vitengo
      • Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ufugaji nyuki
      • Teknologia ya Habari, Mawasiliano na uhusiano
      • Uchaguzi
    • Link ya Machapisho ya Idara/Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kiofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Enviroment and Sanitaion

UTUNZAJI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA

Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati hushirikiana idara zingine kutekeleza shughuli mtambuka zinazohusiana na utunzaji na usimamizi wa mazingira pamoja na udhibiti wa taka ngumu

1.1.Misitu ya Asili na upandaji miti

Katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Babati,kuna aina 2 za Misitu, ambazo ni misitu ya Hiafadhi ya Taifa na Misitu ya Vijiji. Misitu ya hifadhi ya Taifa ni  4 ambayo ni Msitu wa Bereko, Haraa, Ufiome na Msitu wa Nou.

Eneo lote la misitu katika mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya , linakadiriwa kuwa ni hekta 80,000.  Kati ya hizo, hekta 25,871 ni misitu ya Hifadhi ya Taifa ambayo iko chini ya usimamizi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikisha jamii inayozunguka misitu hiyo. Jumla ya hekta 54,129 ni misitu iliyoko katika maeneo ya vijiji na inasimamiwa na vijiji husika. Miti ya asili inayopatikana katika misitu hiyo ni miti aina ya miombo ambayo inafaa kwa shughuli za ufugaji nyuki. Mbinu inayotumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati katika utekelezaji wa kampeni ya upandaji miti ni ushirikishwaji Jamii katika zoezi zima la kuikuza katika vtalu,kuipanda na pia kuitunza miti.  Katika utaratibu huu ,Halmashauri inachangia  nyenzo na ushauri wa kitaalam kwa watu wenye vitalu vya kaya, taasisi, vikundi na vitalu vya vijiji, ili wahusika wenyewe waweze kukuza  miche ya miti katika vitalu vyao na kuipanda katika maeneo.  Kila mwaka, lengo ni kupanda miti 1,500,000 na utekelezaji wake pamoja na kustawi kwa miti inayopandwa ni kati 70% hadi 85% kutegemeana na hali ya hewa ya mwaka husika.   

1.2. Usafi wa Mazingira na udhibiti wa Taka ngumu na

Halmashauri ya Wilaya ya Babati inatekeleza sheria na. ya kufanya usafi wa mazingira kila jumamosi ya mwisho wa mwezi katika kata zote 25 zilizoko katika mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya. Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, viongozi na watendaji ngazi ya kata husimamia na kukagua usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ndani ya kata ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi,maeneo ya biashara, mazingira ya ofisi,minada na maeneo ya magulio. Maelekezo kwa kila kaya ni kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi licha ya kushiriki  zoezi la jumla la mwisho wa mwezi. Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya amefungua jalada maalum la usafi wa mazingira wa kila mwezi kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za usafi wa mazingira za Kata kwa ajili ya uhakiki na ukaguzi wa kushutukiza katika maeneo yanayotolewa taarifa. Halmashauri pia inao mpango wa muda mrefu wa  wa kujenga vizimba vya kudhibiti taka ngumu na kuanisha maeneo ya madampo yasiyopungua eka moja kwa kila eneo katika makao makuu ya Kata zenye idadi kubwa ya watu na zinaokua haraka kuelekea miji midogo. Kwa mwaka wa fedha 2016/17 Halmashauri ilitenga fedha kutokana na mapato ya ndani, na kuwezesha ujenzi wa vizimba 2 katka kata za Gallapo na Dareda na hivyo kuwa na jumla ya vizimba 3 na maeneneo yaliyoainishwa rasmi kama madampo ya kutupa taka ngazi ya Kata.

1.3 Shughuli nyingine za utekelezaji sheria Na.20 ya usimamizi wa mazingira mwaka 2004

Shughuli nyingine za mazingira zinazofanyika ni pamoja na:

  • Kuanisha na kutenga maeneo ya vyanzo vya maji na kuviwekea utaratibu wa utunzaji kwa kushirikisha jamii.
  • Kuelimisha wakulima kuhusu kilimo kinacho zingatia hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na uzuiaji wa makorongo katika maeneo ya kilimo
  • Kuunda nakutoa mafunzo kwa kamati za vijiji zinazosimamia mazingira , kuhusu majukumu yao katika kusimamia mazingira
  • Kuwezesha vijiji kuandaa mpango shirikishi wa usimamizi wa mazingira pamoja na sheria ndogo ambazo hutumiwa na Halmashauri za vijiji kwa ajili ya kudhibiti makosa ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira.
  • Kufuatilia utekelezaji wa sheria ya tathimini ya athari kwa mazingira katika miradi ya uwekezaji inayofanyika ndani ya mamlaka ya halmashauri ya Wilaya
  • Kuendesha  mashindano ya kampeini ya usafi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kuhimiza ujenzi wa vyoo na kuvitumia

       2.0 Changamoto.

  • Pamoja na jitihada zinazofanyika usimamizi na uboreshaji wa mazingira, bado kuna vitendo vya binadamu vinavyofanyika   katika baadhi ya maeneo ya  Halmashauri na kusababisha changamoto za kimazingira ambazo  ni pamoja na;
  • Kupotea au kupungua kwa Bionuai ya asili katika misitu yetu

Fig 1. Uvunaji holela wa misitu    

                   

 Fig 2. Uchungaji holela wa mifugo

  • Ardhi inayotumika kwa kilimo kupoteza rutuba
  • Taka ngumu hususani  aina ya plastiki bado ni tatizo katika maeneo ya mbalmbali na zaidi katika maeneo ya biashara kama vile minada na magulio.
  • Kutoweka,kuingiliwa au kuchafuliwa kwa vyanzo vya maji
  • Madhara mengine yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame na mafurukio
  • Ili kukabiliana na changamoto hizi, pamoja na jitihada zilizokwisha tajwa Halmashauri ya Wilaya inafanya yafuatayo:
  • Kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara katika maeneo lindwa kisheria na kuchukua hatua zinazostahili kwa wavunja sheria za mazingira.
  • Kuendelea na utoaji elimu ya ufugaji bora ili kupunguza athari za kimazingira zitokananazo na  uchungaji huria
  • Kudhibiti uingizaji holela wa mifugo katika maeneo ya Halmashuri ya Wilaya kupitia Halmashauri za vijiji
  • Kuhimiza upandaji wa miti ya asili yenye uwezo wa kuhimili hali ya hewa katika maeneo
  • Kushirikiana na wadau wengine wa mazingira hususan mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayosaidia masuala ya mazingira katika Halmashauri.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA September 25, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI October 03, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WASIMAMIZI VITUO VYA WAPIGA KURA June 30, 2025
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2020 June 17, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Jamii Imetakiwa Kutumia Vyakula Vyenye Virutubisho

    June 24, 2025
  • DAS Matipula. Watumishi Fanyeni Kazi Kwa Bidii

    June 20, 2025
  • Madiwani Waishukuru Serikali Kwa Ujenzi Wa Jengo La Makao Makuu Ya Halmashauri

    June 20, 2025
  • Mkurugenzi Apongezwa Kwa Utendaji Kazi Mzuri

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

MAKALA YA ELIMU IKIANGAZIA SWALA LA TAALUMA NA HALI YA UFAULU KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BABATI
video zaidi

Viunga vya haraka

  • Watumishi portal
  • Lgrcis dashborad
  • Salary silpportal
  • Ramani ya Halmashauri

Tovuti Mbalimbali

  • Tovuti ya Ofisi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Ofisi ya Raisi,Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Wilaya Ya Kiteto
  • Secretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya wilaya ya Babati

    Anwani: P.O BOX 400, Babati.

    Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011

    Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577

    Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani Ya Tovuti

Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.