Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Babati Vijijini Ndg Benedict Ntabagi amewataka Watendaji wa Uchaguzi kufanya kazi kwa bidii, kujituma Ili kufanikisha maandalizi na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba. Msimamizi huyo ameyasema hayo leo kwenye mafunzo ya wasimamizi wasaidiziwa uchaguzi ngazi ya Kata yanayofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ayalagaya. " Nyinyi Watendaji wa uchaguzi kafanyeni kazi kwa bidii ili kufanikisha uchaguzi mkuu amesisitiza kiongozi huyo.Aidha amewaomba baada ya mafunzo kwenda kuanza kutoa Elimu ya mpiga Ili wananchi washiriki kwa wingi kupiga kura katika maeneo yao. Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani unategemea kufanyika tarehe 29.10.2025
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.