Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wametakiwa kuitisha na kufanya mikutano na Vikao Vya kisheri ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima katika maeneo yao. Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Eng Raymond Mushi kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri la Wilaya ya Babati ambao umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Akitoa taarifa za Serikali kwenye Mkutano huo amesema"Mikutano na Vikao vyote vya kisheria vya Vijiji na Vitongoji lazima vifanyike, Wenyeviti wa Vijijini na Vitongoji wasioitisha Vikao wachukuliwe hatua" amesisitiza Mkuu wa Wilaya. Aidha amesisitiza wajumbe wa Baraza la Madiwani kuhamasisha wananchi kutunza vyanzo vya Maji na kuhimiza Halmashauri kuongeza juhudi za ukusanyaji wa Mapato ya ndani ili kutimiza malengo yaliowekwa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Wajumbe wa Mkutano huo kwa pamoja wamesisitiza Vifaa vya upimaji ardhi vinunuliwe mwaka huu ili kupunguza migogoro ya ardhi katika maeneo yao
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.