Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Daniel Sillo amelipongeza Shirika la So They Can (STC) kwa kushawishi ubalozi wa Japan na kupata fedha kiasi Cha Tsh 269,285 395 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule ya Msingi Org'ardida kata Qash,Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mhe.Sillo ameyasema hayo leo alipotembelea shule hiyo na kuona hatua za ujenzi zinazoendelea " Tunawashukuru Shirika la So The Can kwa kazi nzuri wanazendelea kufanya katika Halmashauri yetu Mpaka tunapoona mradi mkubwa unaofadhiliwa na Ubalozi wa Japan katika shule hii wote kwa pamoja STC na Ubalozi wa Japani nchini Tunawashukuru sana" amesisitizi kiongozi huyo. Aidha Mhe. Sillo ameomba Mkurugenzi Mtendaji wa H/Wilaya Anna Mbogo kusimamia mradi huo ili ukamilike kwa wakati na uanze kutumika. Naye Mwenyekiti wa H/ Wilaya John Noya amesema mara baada ya kukamilika mradi huo miundombinu yote ya Madarasa, vyoo na vifaa vyote visimamiwe na vitunzwe vizuri.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.