Wananchi wa Kijiji cha Mamire Kata ya Mamire Halmashauri ya Wilaya ya Babati wamepongeza Serikali kwa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji . Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Endagile Ramadhani Sokola leo kwenye hafla ya kuweka jiwe la ufunguzi la Zahanati hiyo. Mgeni Rasmi wa hafla hiyo Anna Mbogo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati amewapongeza Wananchi wa Kijiji hicho kwa michango na kutoa nguvu kazi katika ukamilishaji wa Zahanati hiyo na kuwaeleza kuwa kwa kuanzia ameisha leta watumishi wawili na vifaa ili zahanati hiyo ianze kutoa huduma. Awali katika Risala ya Wananchi Kwa mgeni Rasmi iliyosomwa na Albetina Mpayo Mtendaji wa Kijiji hicho amesema kufunguliwa Kwa Zahanati hiyo katika Kijiji hicho ni mkobozi kwani wagonjwa, mama wajawazito walikuwa wakitembea kilometa 8 hadi 10 kufuata huduma za matibabu makao makuu ya Kata ya Mamire na sasa huduma hizo zitapatika karibu Katika Hafla hiyo Wananchi walionekana wenye furaha na kushangilia huku wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Babati Anna Mbogo Kwa kuwapa ushirikiano mkubwa Mpaka Zahanati hiyo kukamilika. Ujenzi wa Zahanati ya Endagile umetumia kiasi Cha Tsh 156,000,000 na inategemea kuhudumia Wananchi 1286 wa Kijiji hicho .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.