Naibu Spika ambae ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mh. Daniel Barani Sillo amewaasa Madiwan waonyeshe njia,ushirikiano na mshikamano katika
Kusimamia vema huduma za jamii
Usimamizi mzuri wa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Pia ametoa salam za Mh. SALOME MAKAMBA ambae ni Naibu Waziri wa Nishati na kueleza kwamba Mh.SALOME MAKAMBA amejitolea kuwa mlezi wa jimbo la babati vijijini na amewaaagiza viongozi kuorodhesha vitongoji visivyo na umeme na kuwasilishwa kwa ajili ya uunganishwaji wa nishati hiyo mara moja.
Sambamba na hayo Mh Naibu Spika ameeleza vipaumbele vyake katika jimbo lake la babati vijijini ambavyo ni Umeme, Maji, na Barabara kwani ndivyo vinagusa maisha ya mtu mmoja mmoja na kueleza kwamba huduma nyingine pia zitazingatiwa kutolewa kwa ufanisi
Pia ameeleza Ofisi zake zote kuwa na makatibu ambao watasikiliza kero za wananchi pindi anapokua vikaoni
Amemaliza kwa kusisitiza kutunza Amani ya nchi yetu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.