Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Jacob Twange ameagiza H/Wilaya ya Babati kuweka mkazo ktk ukusanyaji wa mapato ya ndani na kubuni vyanzo vipya ilikupata fedha za kutosha kukamilisha miradi. Mhe Twange ameyasema hayo leo kwenye kikao cha Watumishi wa H/Wilaya ya Babati alipowatembelea leo Makao Makuu ya Halmashauri Dareda kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo."Leo nimekuja kujitambulisha kwenu, lakini wekeni mkazo ktk kukusanya mapato ya ndani na fedha hizo zitumike kulingana na vipaumbele mlivyojiwekea na zifuate taratibu na kanuni za matumizi ya fedha" amesisitiza kiongozi huyo.Aidha ameagiza wakuu wa Idara kusimamia miradi inayotekelezwa kukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.