Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Mhe.Queen Sendiga, amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi nane (8) itakayopitiwa na Mwenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati.Ziara hiyo imefanyika leo, July 03,2025. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati ambapo miradi nane imeweza kukaguliwa.Miradi hiyo iliyokaguliwa ni mradi wa Kituo Cha Afya Gallapo, mradi wa jokofu na kitanda Cha kuoshea maiti, mradi wa daraja Mamire,mradi wa ghala, mradi wa nishati safi na salama, mradi wa maji, mradi wa shule ya wavulana Manyara mradi wa usafirishaji wa kikundi Cha Bajaji Cha Magugu.Ambapo jumla ya gharama ya miradi yote ni tsh. 6,807,344,176.Mhe.Sendiga amesisitiza usafi maeneo yote ya miradi uzingatiwe pia kuongeza miti ya kivuli kwenye miradi husika.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.