Ujenzi wa Nyumba za Walimu katika Shule ya ya Sekondari ya Manyara Boys wavutia watu wengi wanaopita katika eneo la ujenzi wa mradi.Shule hiyo inayojengwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa gharama ya TSH 4.1 Billioni imekuwa kivutio katika Barabara kuu iendayo Arusha ukitokea Babati mjini. Shule hiyo inajengwa Kijiji Cha Ngoley Kata ya Mwada Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo ambaye ni msimamizi mkuu wa ujenzi Shule hiyo ameshukuru Serikali ya Awamu ya Sita Kwa ujenzi wa Shule hiyo Mpya ya kisasa ambayo itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano July 2025. Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Cha Ngoley Ndg Fedelis Molomba wa Kata ya Mwada anashukuru Serikali ya Awamu ya Sita Kwa ujenzi wa Shule hiyo anasema faida za ujenzi wa mradi huo ni nyingi kuanzia ngazi ya kaya kwani wananchi wengi wamepata ajira za muda mfupi na muda mrefu na watoto wao watapata Elimu karibu kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.