Jamii imetakiwa kuchanganya unga wa mahindi na virutubishi ili kutoa mlo wenye lishe Bora kwa watoto. Hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa H/ Wilaya ya Babati Ndg January Bikuba kwa Niaba Mkurugenzi Mtendaji leo kwenye tathmini ya utekelezaji wa mradi wa majaribio wa kuchanganya unga wa Mahindi na Virutubishi iliyofanyika katika Shule ya Msingi Dareda Kati. Ndg. Bikuba amesema suala la lishe Bora ni la Msingi sana kwa watoto wote wanaendelea kukua na lishe ni kichocheo cha Maendeleo ya Watu na Taifa Kwa ujumla, hivyo Kila jamii ilipe kipaumbele amesisitiza kiongozi huyo. Kwa upande wake Ndg. Archard Ngemela Mratibu kutoka Shirika la Gain(Global Alliance for Improved Nutrition) na Youngson Mgogo Mratibu wa Lishe Taifa wameshukuru Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kukubali kutekeleza mradi huo kwa majaribio na kusisitiza jamii ishiriki kikamilifu ili kuhakikisha watoto katika Shule zote wanapata chakula chenye lishe Bora na virutubishi vinavyotakiwa ili kujenga jamii Bora. Naye Afisa Elimu H/ Wilaya ya Babati Getrude Kavishe ameshukuru Shirika la Gain na TAMISEMI kwa kuleta mradi huo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati na kuahidi vifaa, mashine vitatunzwa na watoto katika Shule zilizopo kwenye mradi kuanza kutumia virutubishi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.