Wanafunzi 9522 wa darasa la Saba katika H/Wilaya ya Babati wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka 2022. Afisa Elimu yaMsingi Getrude Kavishe amesema hayo leo ofisini kwake kuwa kati ya wanafunzi hao wavulana waliosajiliwa ni 4432 na wasichana 5090. Aidha ameiomba jamii kuwaruhusu watoto wote waliosajiliwa kwenda kufanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi bila kikwazo chochote. Pia ameleza kuwa mpaka Sasa maandalizi ya kufanyika kwa mtihani huo yanaendelea vizuri katika Shule zote 145 zitakazofanya mtihani huo hapo kesho
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.