Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara wameshukuru Madiwani kwa kazi nzuri ya kusimamia na kutoa ushauri mzuri mpaka Halmashauri kupata mafanikio makubwa kwa Kipindi chote cha miaka mitano.Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo leo kwenye Mkutano wa Baraza Maalum la kuvunja Baraza la Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa H/Wilaya ya Babati.Akisoma mafanikio hayo Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo amesema kwa Kipindi cha miaka mitano imefanikiwa kununua magari 7 kupitia mapato ya Ndani na kupeleka fedha za miradi ya asilimia 40 kila Mwaka Kwa asilimia 100,Kupata Hati safi kwa miaka 5 mfululizo,kupeleka magari mawili ya Wagonjwa katika kituo Cha Afya Nkait na Gallapo.Kwa Upande wake Mwenyekiti wa H/Wilaya ya Babati Mh.John Noya Kwa niaba ya Madiwani amewashukuru Watumishi Kwa ushirikiano wao waliounesha kwa Kipindi chote cha miaka mitano mpaka kupata mafanikio makubwa ya kujivunia na kusisitiza kuendelea kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wa Shule za msingi kwa asilimia 100.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.