Waajiri wametakiwa kusimamia maadili na na kutatua changamoto za Watumishi kwa wakati ili kuleta ufanisi mahali pa kazi. Mhe Regina Qwaray Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ameyasema hayo leo katika kikao chake pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Taasisi zilizopo kilichofanyika katika Ukumbi wa shule ya Sekondari ya Ayalagaya." Waelekezeni kila mara watumishi wafuate maadili ya Utumishi wa umma atakayekiuka achukuliwe hatua za kiutumishi kwa kuzingatia Sheria,taratibu na kanuni za Utumishi wa Umma na maamuzi yote yazingatie haki." Amesisitiza kiongozi huyo. Mhe. Qwaray ametumia nafas hiyo kuwashukuru wanawake wote wa Mkoa wa Manyara Kwa kumchagua kuwa Mbunge na kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Naibu Waziri.Katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati na Kamati ya Ulinzi na usalama, watumishi wameomba vitendea kazi kv pikipiki na ajira mpya kwa upande wa kada za Afya hasa Maofisa Afya na mazingira, kwa ajili ya kudhibiti mlipuko wa magonjwa na madaktari wa kinywa na meno kwenye vituo vipya vya Afya ili kuwasaidia Wananchi wenye changamoto hizo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.