Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray amesisitiza Waajiri na watumishi kudumisha ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mafanikio chanya kwa Wananchi na Taasisi kwa ujumla. Mhe. Qwaray ameyasema hayo leo kwenye kikao Cha pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Taasisi za umma zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ayalagaya. "Watumishi katika Taasisi zetu tufanye kazi kwa bidii na tudumishe ushirikiano ili kuleta matunda chanya kwa Wananchi na Taasisi " amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo Mhe Qwaray amekemea viongozi kutumia madaraka yao kukandamiza watumishi mahali pa kazi akisisitiza kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya Utumishi wa Umma. .Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Kaganda ameshukuru Naibu Waziri kutembelea Wilaya ya Babati na kukutana na Watumishi na kusikiliza changamoto ,ushauri na akamueleza watumishi ndani ya Wilaya wana mahusiano mazuri na wanafanya kazi zao kwa Kwa bidii .Kabla ya kutoa hotuba yake Mhe Qwaray amesikiliza changamoto, ushauri na mapendekezo kutoka kwa Watumishi ambayo yote ameyatolea ufafanuzi kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo. Mwisho Mhe Qwaray amesisitiza Watumishi wote nchini kuwa wazalendo katika kulinda maadili ya Utumishi wa Umma.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.