Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Karoline Mthapula ameagiza watumishi kufanya kazi kwa bidii kujituma na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kutoa matokeo chanya kwa wananchi . Hayo ameyasema leo kwenye kikao kazi cha watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kilichofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano " nyinyi kama watumishi wa umma mnatakiwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kuzingatia sheria, kanuni za utumishi wa umma" amesisitiza kiongozi huyo . Aidha Bi Mthapula ameagiza Halmashauri kukusanya mapato ili kuweza kujenga miradi kupitia mapato yake ya ndani na amesisitiza kufanyika kwa vikao vya kisheria ngazi za chini. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati amemshukuru katibu Tawala huyo kwa mafunzo na maelekezo yote na kusema maagizo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.