Ushirikiano na kujituma kati ya Madiwani na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ni nguzo kubwa katika ukusanyaji wa Mapato ya ndani. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Babati Mhe John Noya leo kwenye Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani wa kujadili Rasmi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka fedha 2026/2027. Katika huu wa fedha tunaendelea nao ushirikiano kati ya Madiwani na Wataalamu umezaa matunda katika ukusanyaji wa Mapato, uendelezwe amesisitiza kiongozi huyo" Mhe. Noya ameomba Madiwani kutoa ushirikiano katika maeneo yao kuhakikisha Mapato yote yaliyokisiwa yanakusanywa. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo ameomba Madiwani kuhamasisha amani kuwa ni Msingi wa Maendeleo mahali popote.Baraza la Madiwani linaendelea na kujadili mapendekezo hayo Mpaka yatakapitshwa na kesho na Mkutano wa Baraza.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.