Kituo cha Afya Dareda Kati kilichopo kata ya Ayalagaya Halmashauri ya Wilaya ya Babati kimepokea Waganga wa Wilaya na Waganga Wafawidhi wa Mkoa wa Manyara kwa ajili ya kujifunza. Akiongea na ugeni huo leo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Dkt Hosea Madama amesema lengo la ujio wa ugeni huo ni kwa ajili ya kujifunza mambo mabalimbali hususan maboresho makubwa katika kituo hicho Mf CEMONc yanayofanywa na kituo hicho. Mara baada ya kujifunza na Kutembelea kituo hicho viongozi hao wameshukuru Serikali inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan na wadau wa Maendeleo Karim Foundation kwa uboreshaji mkubwa wa miundombinu, na huduma za Afya katika kituo hicho.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.