Madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Babati, Hanang na Mji wa Babati wametakiwa kufanya kazi kwa upendo na kushirikiana ili kuwaletea Wananchi maendeleo . Hayo yamesemwa leo na Ndg Said Mnenge mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofsi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwenye kufunga mafunzo elekezi ya Madiwani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati "Fanyeni kazi kwa kushirikiana nyinyi na watumishi wa Halmashauri zenu ili kuwaletea Wananchi maendeleo " amesisitiza kiongozi huyo . Wakati huo huo Ndg Mnenge amesisitiza Kila Halmashauri kukusanya Mapato yake ya ndani kulingana na lengo ili Halmashauri ziweze kujiendesha.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe John Noya kwa niaba ya Madiwani wote ameshukuru Serikali, inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania viongozi wa Halmashauri zote kwa mafunzo hayo akisema yatasaidia sana madiwani kufahamu majukumu na mipaka yao, Maadili,Sheria za Serikali za mitaa, vyanzo vya Mapato na Maandalizi ya Bajeti katika ngazi za msingi,. Mafunzo elekezi kwa Madiwani yamehitimishwa leo na yalikuwa yanatolewa na Wakufunzj kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.