Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg.Veronica Marwa amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidii kutekeleza majukumu yao ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Halmashauri hiyo.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ameyasema hayo wakati wa kikao Maalumu cha Baraza la Wafanyakazi cha Kujadili Bajeti ya Halmashauri ya mwaka 2017/2018"Sisi kama viongozi tunatakiwa kujitoa kuwatumikia watumishi wenzetu na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya bila kujali tunapata nini" Alisisitiza Kaimu Mkurugenzi Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji aliwaeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa Baraza la wafanyakazi lipo kisheria kujadili changamoto zinazojitokeza mahali pa kazi na kuzitatua hivyo,akawataka Viongozi wanapokutana na changamoto wasisite kuwasiliana na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji. Baraza hilo limepitisha jumla ya makisio ya Tsh 38,704,002,280 kwa bajeti ya mwaka 2017/2018 kuendelea kujadiliwa kwenye vikao vingine kishakuwasilishwa Wizarani.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.