Watendaji wa Kata na Vijiji katika H/ Wilaya ya Babati wamesisitizwa kusimamia Ukusanyaji wa mapato ya serikali yatokanayo na uchinjaji wa Mifugo na minada katika maeneo yao. Hayo amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Ndg Benedict Ntabagi katika kikao kazi Cha Watendaji wa Kata na Vijiji kilichofanyika leo Ktk ukumbi wa H/Wilaya Arri, "Kila mmoja Ktk maeneo yake asimamie Ukusanyaji wa mapato ya serikali yatokanayo na uchinjaji wa Mifugo na minada" "amesisitiza kiongozi huyo . Aidha Mkurugenzi huyo amesisitiza watendaji hao kufuata kanuni ,taratibu na Sheria katika matumizi ya fedha na kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa kwenda banki kwanza kabla ya matumizi . Watendaji hao pia wamesisitizwa kufanya vikao vya kisheria katika maeneo yao na katika vikao hivyo taarifa za mapato na matumizi zisomwe na kuwasilishwa Kwa Wananchi.H/ Wilaya ya Babati imeweka utaratibu Kila baada ya robo mwaka kukaa na watendaji hao kukumbushana wajibu na majukumu yao ili kuwaletea maendeleo Wananchi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.