Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewaomba Wananchi kulinda na kutunza miradi inayojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Wananchi ili iweze kuleta maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo. Hayo ameyasema leo Ktk Hospitali ya H/ Wilaya Mwada mara baada ya kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira Ktk eneo hilo ikiwa ni kuelekea kilele Cha Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru trh 9/12. " Miradi yote inayojengwa Ktk maeneo ya vijijini ulindwe na kutunzwa"
amesisitiza kiongozi huyo huku akiwaonesha majengo mbalimbali yaliojengwa na Serikali katika eneo hilo. Wakati huo huo Mzee Maarufu Hamisi Babu aliyekuwepo kabla ya Uhuru ameweza kutoa historia fupi ya Uhuru wa Tanzania Bara na kusema Kuna maendeleo Makubwa yamepatikana baada ya Uhuru na akaomba wananchi kufanya kazi Kwa bidii na kutunza mazingira. Katika kuelekea kilele Cha miaka 61 ya H/Wilaya ya Babati inafanya shughuli za usafi wa mazingira,upandaji wa miti,michezo, Sanaa na midahalo mbalimbali kuanzia ngazi za Vitongoji na vijiji.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.