Wananchi wa Kata ya Secheda Wilaya ya Babati wameshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kiasi cha Tshs 584,280,028 za ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Secheda. Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa kijiji cha Secheda Ndg Gabriel Ingi na Diwani wa Kata ya Secheda Ibrahim Tatock kwa nyakati tofauti mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo " Sisi wananchi wa kijiji cha Secheda tunashukuru serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Secheda " wamesisitiza viongozi hao. Diwani wa kata hiyo ameeleza kuwa kupatika kwa shule hiyo kutapunguza adha ya wanafunzi kutembea Km 21 kwenda Shule mama ya Sekondari ya Ufana. Kwa upande wake Mhe. Sendiga amewapongeza wananchi hao kwa kutoa michango kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Zahanati ya Secheda ambapo wananchi wamechangia kiasi cha Tshs 45 Millioni na zahanati hiyo imekaguliwa leo na Mh. Sendiga.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.