Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndugu Anna Philip Mbogo amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za madiwani katika Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani kwa kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi ambapo Halmashauri ilikuwa ikisimamiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Menejimenti mara baada ya Madiwani kumaliza muda wao.
Akiwasilisha taarifa hiyo Ndugu Anna Mbogo ameeleza kwamba kwa kipindi cha mwezi Julai hadi tarehe 27 Novemba 2025 halmashauri imekusanya Tsh 3,701,003,578 sawa na 39% ya makadirio ya mapato yote kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na imetumia Tsh 26,393,974,000 katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli nyingine katika Halmashauri.
Halmashauri imeweza kuajiri madereva 2 na pia imepata kibali cha ajira 231 za kada mbalimbali,halmashauri imeweza kusimamia nidhamu za watumishi na kusikiliza mashauri mbalimbali,halmashauri imeweza kulipa stahiki mbalimbali za watumishi na viongozi wa kisiasa, kuratibu vikao vya kisheria katika ngazi za kata na vijiji na kuratibu shughuli za uchaguzi mkuu.
Sambamba na hayo halmashauri iliweza kusimamia utekelezaji wa shughuli zote katika vitengo na divisheni zake, katika divisheni za elimu mitihani yote iliratibiwa na kufanyika kwa usalama.
Pia halmashauri iliweza kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, utoaji mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali pamoja na kuratibu shughuli za TASAF.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.