Wananchi wa kitongoji cha Endabanyeq katika kijiji cha Gidewari Kata ya Dabil Halmashauri ya Wilaya ya Babati wameomba Mkuu wa Wilaya ya Babati na Mkuu wa Wilaya ya Hanang kwenda kufanya Mkutano wa ujirani mwema katika eneo linalopatika madini ya chumvi katika kitongoji chao. Wananchi wameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika eneo linalopatikana chumvi na nakuhudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg. Halfan Matipula Wakati alipotembelea kitongoji hicho kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzitatua. Wananchi hao wamemueleza katibu Tawala kuwa wanachangamoto ya barabara, Shule ya Msingi shikizi,ofisi na Uongozi katika eneo linalopatika madini ya chumvi . Akijibu hoja zao Matipula amewaleza Wananchi hao kuwa malalamiko yao yatafanyiwa kazi haraka na kuwasisitiza Wananchi hao kufanya kazi kwa bidii na kuishi kwa amani na majirani zao wa Hanang. Kitongoji cha Endabanyeq ni Maarufu Kwa uzalishaji madini ya chumvi katika H/ Wilaya ya Babati
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.