Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe . Queen Sendiga amewataka Madiwani kuwatembelea , kuwasikiliza na kutatua changamoto za Wananchi katika maeneo yao. Mhe Sendiga ameyasema hayo leo kwenye Ufunguzi wa Mafunzo elekezi ya Madiwani wa Halmashauri za Hanang, Babati Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Babati yaliyofanyika leo katika Ukumbi wa Hamashuri ya Wilaya ya Babati. " Tembeleni Wananchi wasikilize na tatua changamoto zao amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo huo Mhe Sendiga amewataka Madiwani kusimamia huduma za kijamii kila siku katika maeneo yao akisema Diwani ni mwakilishi wa Mhe Rais katika kata yake hivyo anawajibu wa kuhakikisha kusimamia kata yake na kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia Wananchi wote bila ubaguzi.Katika hotuba yake ya Ufunguzi Mhe Sendiga amewaasa viongozi hao kujiepusha na masuala ya Migogoro hasa Migogoro ya ardhi akisema katika Mkoa wa Manyara migogoro haina tija inarudisha maendeleo ya wananchi nyuma. Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Wahe. Wakuu wa Wilaya wa Babati na Hanang, Makatibu Tawala na Wakurugenzi watendaji Hanang , Babati na Kaimu mkugenzi wa Mji wa Babati. Mafunzo ni ya siku mbili na yanatarajia kumalizika kesho.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.