Kata za Gallapo, Magugu na Ayasanda katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara zashinda katika mashindano ya usafi wa Mazingira (SRWSS) kwa mwaka 2024/2025 chini ya Kampeini ya "Mtu ni Afya". Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe. John Noya kwenye wa mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika leo katika Ukumbi wa H/Wilaya ya Babati. " Kati ya kata 25 ni kata tatu za Gallapo. Magugu na Ayasanda ambazo zimeshinda kwenye Kampein ya Mtu ni Afya. Kwa mwaka tajwa Hongereni sana" amesisitiza. Wakati huo huo Mhe. Noya amezitaka kata nyingine kukazana ili wakati mwingine zifanye vizuri.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.