Halmashauri ya Wilaya ya Babati imepata gari jipya kwa ajili ya kufuatilia miradi ya maendeleo na shughuli za utawala Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji. Akitambulisha gari hilo leo kwenye kikao Cha Timu ya Menejiment, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Babati Anna Mbogo alisema "Serikali kuu imetuletea gari lenye Na. Sm 44487 kwa ajili ya shughuli za Utawala, Tunamshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutupatia gari hilo" amesisitiza kiongozi huyo. Gari lenye Na SM44487 limefika wakati mzuri ambao Halmashauri ina shghuli nyingi za ufuatliaji miradi na Utawala.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.