Wanafunzi waliomaliza kidato cha Nne 2025 na walimu wote waliowafundisha wa Mkoa wa Manyara wamepongezwa kwa kufanya vizuri na kushika nafasi ya pili Kitaifa. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa Mhe Queen Sendiga leo kwenye Ufunguzi wa Mafunzo elekezi ya Madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Hanang, Babati Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Babati yaliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati " Ni ukweli usipingika wanafunzi waliomaliza kidato Cha Nne 2025 na walimu wao wametuheshimisha" , Hongereni sana amesisitiza kiongozi huyo.Katika kikao hicho Mhe Sendiga amesisitiza maagizo Waziri Mkuu Mhe Mwigulu Nchemba wa kuanzia sasa Kila Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa na amesisitiza viongozi hao kuendelea kutoa Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.