Wananchi wameshauliwa kuyapuuza maneno ya uchonganishi kuwa serikali ya awamu ya Tano haiwasaidii Wakulima.Hayo ameyasema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Será Bunge ,Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama leo wakati akitembelea na kukagua Miradi iliyojengwa na Programu ya MIVARF ambayo ni ujenzi wa Ghala, Barabara Km 9 , Madaraja 2 , Box kalvati 3 na Mashine ya kusindika Mpuga zenye thamani ya Tsh 1.2 Bilioni iliyojengwa
katika Halmashauri ya Wilaya Babati kata ya Magugu Vijiji vya Matufa na Masware. "Nimekuja kukagua miradi iliofadhiliwa na MIVARF kupitia ofisi yangu nimeona kwa macho yangu miradi hiyo ni Mizuri itunzeni na fanyeni kazi kwa bidii na Ole wenu miradi hiyo isipokuwa endelevu" amesisitiza Mhe. Waziri. Aidha ameshukuru uongozi wa Halmashauri Wilaya ya Babati kwa kuweza kuchangia Tsh 63,621,855 ambazo ni asilimia 5 ya Gharama za utekelezaji wa Mradi kama Mwongozo ilivyoelekeza.Pia Mhe.Waziri ametembelea Bank ya CRDB tawi la Magugu ambapo ameshauri jinsi gani wanaweza kupunguza riba ya Mikopo kwa wajasiriamali wadogo , Kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo na kufunga dirisha Maalumu lá kukopesha Vijana na Wanawake.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.