Wananchi wa Kata ya RIroda Halmashauri ya Wilaya ya Babati wameishukuru serikali kwa kuwapatia umeme hadi kwenye vitongoji. Wananchi wameyasema hayo leo kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange uliofanyika katika Shule ya Sekondari Chief Dodo wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi " Tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta umeme mpaka kwenye vitongoji " Wananchi wamesikika wakisema kwenye mkutano huo . Mhe Twange akiongozana na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, RUWASA, TARURA, TANESCO wameshirikiana kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Wakati huohuo Mhe Twange amepiga marufuku wananchi wanaojichukulia sheria mkono na kuagiza waalifu wote wapelekwe kwenye vyombo vya dola. Mhe Twange anaendelea na ziara mbalimbali kwenye Tarafa na kata kusikiliza na kutatua kero ambapo wananchi wametatuliwa changamoto zao.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.