Wananchi wa Kitongoji cha Maweni kijiji cha Endadosh Kata ya Qash H/Wilaya ya Babati wamemshukuru Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujenzi wa mradi wa kusambaza maji hadi shule ya Msingi Malesh kijiji cha Endadoshi. Hayo yamesemwa na Halili Juma Mwenyekiti wa Tawi la CCM Endadoshi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM ya Wilaya ya Babati leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM" Tunashukuru sana Serikali ya Mama Samia kutuletea Maji hadi kijiji cha Endadoshi ameongeza. Wakati huo huo wananchi wamemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Lazaro Twange kwa usimamizi wa mradi huo. Naye Mhe Twange amesema shukurani hizo ziwafikie BAWASA, Mbunge wa jimbo la Babati vijiji Mhe Daniel Sillo, TANROAD ,Uongozi wa H/Wilaya, wananchi kata za Gallapo na Qash waliowezesha mradi huo kukamilika. Mwenyekiti wa CCM wilaya Babati Vijiji Mhe Jackson Haibei amesisitiza wananchi kutunza mradi huo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.