Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Mamire Kata ya Mamire H/ Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wameshukuru Serikali kurudisha Mpango wa kunusuru Kaya masikini TASAF awamu ya pili. Mwenyekiti wa kijiji hicho Mhe.Hamisi Maulid kwa nyakati tofauti katika Kikao cha H/ Kijiji na Mkutano Mkuu wa utambuzi na uandikishaji wa Kaya za Walengwa, uliofanyika leo katika viwanja vya ofisi ya kijiji hicho, kwa niaba ya Wananchi amesema " Tunashukuru serikali yetu ya awamu ya sita kwa kurejesha mpango wa kunusuru Kaya Masikini TASAF kwani ilikuwa hitaji la Wananchi wa kijiji cha Mamire la muda mrefu " amesisitiza kiongozi huyo. Naye Marietha Sanka Mkazi wa Kitongoji cha Mamire kati katika kijiji hicho ambaye ametambuliwa na kuandikishwa kuwa mlengwa wa Kaya Masikini ameshukuru serikali kuanzisha mpango huo na kusema '' Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendeleza mpango huo".amesisitiza mama huyo. Kwa mwaka huu ni vijiji 39 vya H/Wilaya ya Babati vilivyoingizwa kwenye mpango huo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.