Wananchi wa Kata ya Madunga H/ Wilaya ya Babati wameshukuru Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia fedha kiasi Cha Tsh 250,000,000 za Awamu ya pili kwa ajili ya ujenzi wa majengo Matatu ya kituo hicho. Akisoma taarifa ya ujenzi wa majengo hayo leo mbele ya Kamati ya Fedha,Mipango na uongozi ya H/ Wilaya ya Babati wakati kamati hiyo ikiwa kwenye ukaguzi wa miradi ya maendeleo,Mtendaji wa Kijiji cha Gidngwar Ndg Imani Lyimo amesema walipokea fedha za ujenzi wa majengo Matatu mwaka jana ambayo ni Jengo la Mama na Mtoto, jengo la Upasuaji na jengo kufulia ambayo yote yako hatua ya upauzi na yanaendelea vizuri. Makamu Mwenyekiti kamati ya fedha , Mipango na Uongozi Mhe. Yahaya Loya amepongeza Viongozi na Wananchi wa Kata hiyo na kuagiza waendelee kushirikiana mpaka Mradi huo ukamilike Kwa wakati . Kituo hicho kinatumika mpaka sasa na baadhi ya Majengo ya huduma za nje( OPD )na Maabara yamekamilika na yanatumika.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.