Kata ya Secheda iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara imepokea fedha kutoka Serikali kuu wa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari. Akitoa Taarifa ya Serikali kwenye Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati leo iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amesema serikali kuu imetoa fedha Kiasi cha Tshs 584,280,028 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Secheda kupitia mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya Elimu ya Sekondari (SEQUIP) .Naye Diwani wa kata ya Secheda Mhe. Ibrahim Tatock ameshukuru serikali kwa ya Awamu ya sita kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Secheda. " Kwa niaba ya wananchi tunashukuru serikali yetu kwa ujenzi wa shule hiyo ambayo ili kuwa ni hitaji la wananchi kwa muda mrefu" amesisitiza Diwani huyo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.