Mwanafunzi Ushindi Peter Saktay kutoka shule ya Sekondari Magugu H/Wilaya ya Babati amepewa zawadi ya fedha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Makongoro Nyerere baada ya kushinda uandishi wa Insha ya Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika kwa shule za Sekondari kimkoa.Mwanafunzi huyo amepokea zawadi hiyo leo kwenye kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru kimkoa iliyofanyika Uwanja wa Kwaraa Mjini Babati.Aidha Mkuu wa Mkoa amesisitiza wananchi kwenda kuchanja katika vituo vyote vilivyoanishwa ili kujikinga na Virusi vya Corona. " Unapochanja unazuia kiwango kikubwa kupatwa na ugonjwa wa Corona" amesisitiza kiongozi huyo. Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Manyara, wazee maarufu, wazee waliozaliwa tarehe 9/12/1961 na kupambwa na vikundi mbalimbali vya burudani.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.