Wanafunzi wa shule za msingi za Tarafa ya Gorowa katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati,Mkoa wa Manyara wamepata neema ya ufadhili wa vifaa mbali mbali vya michezo zikiwepo jezi,mipira pamoja pampu za kujazia mipira hiyo kwa ajili ya maandalizi ya kuandaa timu bora ya kushiriki ligi ya Umitashumta mwakani. Ufadhili huo umetolewa na shirika la World Vision na kukabidhiwa kwa walimu wa michezo wa shule hizo Septemba 19 mwaka huu.
Akipokea vifaa hivyo Mwakilishi wa walimu na Katibu wa mashindano hayo Mwalimu Hasheem ameshukuru na kusema kuwa watahakikisha wanaendesha ligi hiyo bila kuathiri ratiba za masomo za wanafunzi na watasimamia kanunu zote za ligi ikiwemo kuepuka kufanya mikutano kabla ya mechi,timu zinatakiwa kufika uwanjani nusu saa kabla ya mechi.
Aidha ,Walimu hao wameshukuru kwa ufadhili huo na kumalizia kwa kusema kuwa watahakikisha wanasimamia nidhamu katika michezo yote ,huku ligi hiyo ndogo ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema wiki ijayo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.