Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg. Hamisi Idd Malinga ametengua madaraka ya Walimu Wakuu wa shule za Msingi 28 na Maofisa Elimu Kata 10 kutokana na kutofikia asilimia 50 ya ufahulu wa Wanafunzi katika Mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi mwaka 2017 kwa shule wanazoziongoza. Mkurugenzi huyo ameyasema hayo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati "Tumeamua kutengua Wadhifa wa Walimu Wakuu na Maofisa Elimu Kata kutokana na kufelisha watoto wa shule za Msingi chini ya asilimia 50katika Mtihani uliomalizika mwaka jana" alisisitiza Mkurugenzi huyo.Katika kikao hicho aliwaomba wajumbe kutoa ushirikiano kwa walimu Wakuu wapya watakaoteuliwa ili kuongeza kiwango cha ufahulu kwa mwaka 2018.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.