Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Elizabeth Kitundu ameagiza Shule za Msingi na Sekondari zenye Mashamba yalimwe yazalishe chakula kwa ajili ya Wanafunzi.Hayo ameyasema leo kwenye Kikao cha Wadau wa Elimu wa H/Wilaya kilichofanyika Ukumbi wa Babati day sekondari. "Mashamba yote yalimwe na yazalishe chakula kwa ajili ya Wanafunzi na Wanafunzi hao wafundishwe kulima" amesisitiza kuongozi Hugo aidha ameagiza shule zinazokodisha Mashamba fedha inayopatikana itumike kununulia chakula kwa ajili ya Wanafunzi. Katika kikao hicho Shule zilizofanya vizuri zimepewa zawadi ya cheti cha ushindi na Shule zilizofanya vibaya zimepewa cheti cha Onyo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.