Wajumbe wa kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepongeza H/W ya Babati kwa usimamazi wa ujenzi wa miradi iliyopewa fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVICO_19. Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao na Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini Mhe. Daniel Sillo wameyasema hayo leo katika shule ya Msingi Kazaroho iliyoko katika Kijiji cha Kazaroho kata ya Kisangaji H/ W ya Babati." Tumefurahishwa na ujenzi wa mradi huu mnastahili pongezi" Aidha wajumbe hao wameshauri serikali ya kijiji kuongeza ukubwa eneo la shule na kushauri ofisi ya Rais TAMISEMI inapojenga madarasa ihakikishe inajenga na nyumba za Walimu na kuajiri walimu wengi ili kutatua tatizo la upungufu wa walimu katika shule hizo . Akishukuru kwaniniaba ya wananchi Diwani wa Kata ya hiyo Mhe Adamu Ipingika amesema anaishukuru serikali kwa kuwapatia fedha kiasi cha Tsh 120 Million kwa ujenzi wa madarasa sita na wananchi walijitolea nguvu na vifaa vyenye thamani tsh 6,835,000.madarasa hayo yamekamilika
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.