Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo na Jumuiya wafanya Biashara,Viwanda na (TCCIA) leo wametoa msaada wa vyakula, Mahindi gunia 90 na vitu mbalimbali vya nyumbani kwa waathirika wa mafuriko katika kijiji cha Manyara, Moya na Magara katika kata ya Magara.Mhe.Twange akiwa kijiji cha Manyara ametoa pole kwa wananchi wote wa kata ya Magara kupatwa na mafuriko na kuharibiwa na makazi na vyakula katika maeneo yao na kusema Serikali ipo pamoja na wananchi wote waliopata mafuriko na itaendelea kuwasaidia.Naye Diwani wa kata ya Magara Mhe. Jacob Bilkuli ameshukuru Serikali kuu Halmashauri, Mbunge Daniel Sillo kwa kutoa misaada tangu mafuriko yametokea na kuomba ushirikiano huo uendelee.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.