Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewataka viongozi wa vyama vya siasa kufanya kampeini safi za kistaarabu zenye kujenga hoja na kudumisha amani ya nchi yetu wakati wote wakuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27/11/2024. Hayo ameyasema leo wakati akitoa maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wadau mbalimbali kikao kilichofanyika katika ukumbi wa H/ Wilaya ya Babati " Hakuna nchi nzuri kama Tanzania, katika kipindi hiki cha uchaguzi fanyeni kampeni nzuri zenye kujenga hoja na kudumisha amani" amesisitiza Kiongozi huyo . Wakati huohuo Katibu Tawala Wilaya ya Babati Halfan Matipula amesisitiza viongozi wa vyama kuheshimiana na kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. Maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa yametolewa leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vya siasa, Viongozi wa Taasisi wasimamizi ngazi za Kata na vijiji .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.