Watu wenye mahitaji maalum 30 kutoka Vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Babati wamepatiwa viti mwendo na shirika lisilo la Serikali la Chair for love ( kutoka Marekani) kwa kushirikiana na Chemchem Association yenye Makao makuu yake katika kata ya Nkait. Wakipokea viti hivyo na kuvigawa kwa wahusika leo katika Makao Makuu ya Halmashauri, Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg Halfan Matipula,Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Babati John Noya na Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo kwa pamoja Wamewashukuru mashirika hayo kwa kutoa viti kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
"Tunawashukuru sana kwa ufadhiri huo na ushirikiano huo uendelee" wamesisitiza viongozi hao. Naye Mwajuma Omari kwa niaba ya wanufaika ametoa shukurani kwa mashirika hayo na kusema msaada huo utawasaidia kwa kiwango kikubwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ameshukuru Mashirika hayo na kusisitiza wanufaika wa viti hivyo kuvitunza ili viweze kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.