Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harrison Mwakyembe,amewataka Viongozi wa Taasisi za Serikali kushirikiana na Waandishi wa Habari kutoa Habari kwa umma ili Wananchi wafahamu kazi zinazofanywa na Serikali yao. Akiongea na Wadau wa Habari katika Ukumbi wa H/Wilaya ya Babati ya zamani leo amesema inasikitisha kumkuta Mkuu wa Taasisi ya serikali hataki kutoa habari kwa Waandishi wa habari ili ziandikwe na zifahamike kwa Wananchi wote" amesisitiza kiongozi huyo na kusema kutoa habari ni takwa la kikatiba Ibara ya 18 kila mtu ana haki ya kupata habari kuhusu jambo lolote linalofanyika katika nchi yake.
Wadau wa Habari wakisikiliza kwa makini nasaha za Mh Waziri
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Magufuli imefanya mambo mengi mazuri hakuna cha kuficha, vitangazwe vyote Wananchi wafahamu,ameongeza Dkt Mwakyembe.Aidha amesisitiza Waandishi wa Habari kuandika habari za kweli,zenye uhakika zenye kuzingatia taaluma na maadili ya Uandishi wa habari na kusisitiza hakuna Uhuru usiokuwa na Mipaka.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.