Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni wametoa mabati 230 kusaidia jitihada za wananchi wa Kata ya Gallapo katika ujenzi wa jengo la Upasuaji kituo cha Afya Gallapo. Aidha katika kusaidia jitihada hizo Wabunge wa Mkoa wa Manyara wakiongozwa na Mbunge wa Hanang Mhe. Dkt Mary Nagu wamechangia Tsh 1,400,000. Mhe Diwani wa Kata ya Gallapo amechangia Tsh 100,000 na wananchi wengine kuchangia mifuko ya simenti, Jengo hilo limefikia hatua za upauzi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.