"Viongozi,kuweni makini, acheni undugu, ubinafsi na mtende kazi zenu kwa haki na uaminifu katika utambuzi na uandikishaji walengwa wa mpango wa Kaya Maskini TASAF". Hayo yamesemwa na Diwani wa Kata ya Endakiso Mhe.Hasani Omari Dodo kwenye Mkutano wa utambuzi na uandikishaji wa walengwa wa Kaya masikini uliofanyika leo ktk viwanja vya ofisi ya kijiji cha Endakiso kata ya Endakiso H/Wilaya ya Babati.Aidha Diwani huyo ametoa pongezi kwa serikali Kuu na H/Wilaya ya Babati kwa kukubali kijiji hicho kuwekwa kwenye mpango wa TASAF wa kunusuru Kaya Maskini mwaka huu na akawataka wananchi watakao bahatika kuwa kwenye mpango huo kutumia fedha vizuri ili ziwaletee maendeleo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.