Wajumbe wa Mpango wa Elimu changamani kwa vijana (IPOSA) nchini kutoka Wizara ya Elimu,TAMISEMI ,Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima,na Wafadhili kutoa Korea wamepongeza H/ Wilaya ya Babati kwa kupokea mpango na hatua za ujenzi wa karakana katika kituo cha Bashnet kata Bashnet .Hayo yamesemwa na Dr.Sempeho Siafu mratibu wa mradi huo nchini leo walipotembelea karakana na kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo " Tunamshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa ushirikiano na utekelezaji wa mradi hadi hatua ya mradi ilipofikia tunaimani mradi utakamilika kwa wakati na kutoa huduma iliyokusudiwa" Aidha Viongozi hao wamepongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dr Samia Suluhu Hassan Kwa uongozi Bora ulioleta Maendeleo kwa wananchi.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati amepokea Viongozi wa IPOSA kutoa Kutoka Wizarabya Elimu, TAMISEMI, na Taasisi ya Elimu ya watu Wazimak utoka korea Korea
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.