"Afya ni kila kitu, Afya haina mbadala, wote tushirikiane kutokomeza magonjwa ya Mlipuko" Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Lazaro Twange leo kwenye Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ( PHC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa H/Wilaya ya Babati. Mhe Twange ametoa kipindi cha Miezi mitatu kila kaya iwe imechimba , kujenga choo bora na kukitumia ili kuepuka magonjwa ya mlipuko baada ya muda huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa kaya husika. Wakati huohuo Mhe. Twange ameagiza viongozi ngazi zote kushirikiana kutokomeza ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ,"Wale ambao wanafanya vitendo vya ukatili wa kijinsia toeni taarifa haraka ili hatua za kisheria zichukuliwe". Mhe Twange ameshukuru Wadau wa Afya kwa kazi nzuri wanazofanya kwenye Vijiji ili kutokomeza magonjwa ya mlipuko.Kikao hicho kimehudhuriwa Viongozi wa Dini, Wadau wa Afya ( USAID Afya yangu) kamati ya Ulinzi na usalama na viongozi kutoka Wizara za Afya na TAMISEM na viongozi wengine kutoka kwenye vijiji na kata .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.